HOME

Wednesday, 4 January 2017

JINSI YA KUIFANYA FLASH DISK IWE BOOTABLE

Habarini ndugu zetu, leo tunajifunza namna ya kuifanya flash kuwa bootable,

Hii njia mara nyingi hutumika pindi CD-ROM ya computer yako inapokuwa imeharibika, ama computer yako haina CD-ROM, na wakati mwingine ni kwa uharaka wa kufanikisha operating system installations.

Kuna kuweka Bootable kwa ajili ya windows 7/vista ni rahisi zaidi, lakini pia ni tofauti kwa windows xp, na pia nitofauti kwa Ubuntu/linux

http://www.datarecoverybd.com/wp-content/uploads/2015/03/51exav.png

Flash kuwa bootable maana yake ni kuweza kuBOOT computer baada ya BIOS INTERFACE, hii ni kwa ajili ya computer zilizokufa operating systems/ama unapenda kuchange OS 

Hii hapa ni njia rahisi ya kuifanya FLASH kuwa Bootable kwa windows 7/vista
1. Open Command Prompt , hii unaweza kuipata kwa ku bonyeza "start" alafu andika CMD
2. Ikifunguka Andika DISKPART
3. Then ikiisha funguka andika LIST DISK
4. Then Utapata machaguo mbali mbali ya disk zilizopo/zilizokuwa connected kwenye computer
NOTE: disk 0 = internal hard disk
disk1= USB flash
disk2=USB flash or other
Inategemeana na umeconnect flash ngapi
5. Then andika "SELECT DISK 1" kutokana na disk namba ya USB flash yako
6. Then Andika "CLEAN"
7. Then Andika "CREATE PARTITION PRIMARY"
8. Then Andika " ACTIVE"
9. Then Andika "FORMAT FS=FAT32 QUICK"
10. Ikimaliza Andika "EXIT"

SASA BAADA YA HAPO????
Tumia Software yoyote ile kucopy file za operating system hasa windows 7/vista, Ila hapa complex system tuna recommend tumia "POWER ISO" kuextract windows Files (NimeATTACH unaweza ukaidownload.)

http://imag.malavida.com/mvimgbig/download/poweriso-921-1.jpg

No comments:

Post a Comment