Unaweza kujitengenezea kipato wewe mtanzania kwa kujiajili katika shughuli mbalimbali,Sio lazima uajiliwe katika makampuni makubwa ama serikalini ama mahala popote bali unaweza ukabuni namna yoyote ya kutengeneza kipato na kutimiza ndoto zako, Kwako mwanafunzi unae maliza chuo sasa ama uliepo nyumbani tu una computer yako ila una shindwa utaanza vipi kujikimu kimaisha hii ni fursa yako sasa kujua jinsi ya kuandaa Operating system (OS) na kufanya installation katika Computer yoyote.
Kuna njia mbali mbali za kuweza kuweka Operating system (OS) katika computer yako leo nitakupa Njia mbili ambazo ni rahisi Zaidi kwako.
Katika njia zote hizo ni kwajili ya Windows 7 zote pamoja na Windows 8 zote
VIFAA VYA KUWA NAVO KABLA HUJAANZA CHOCHOTE
Kwa njia ya kwanza hakikisha una flash Drive ambayo itakulazimu uifanye kuwa bootable bila ya kufanya hivo itakuwa sio rahisi kukamilisha zoezi lako isipo kuwa kama computer yako itaweza ku boot hivo hivo,Je utaifanya vip Flash yako iweze ku boot
POWER ISO
Power Iso ni software inayo weza kukusaidia kutengeneza flash iweze ku boot unaweza kupata software hiyo kwa kubofya hapa http://www.poweriso.com/thank-you.htm
Kabla ya kuaandaa flash yako kumbuka window 7 au 8 itakuwa katika muonekano huu
Hakikisha ina kuwa katika mfumo wa image kama picha inavo onesha hapa chini
Baada ya kufungua software ya power Iso copy mafile ya windows na paste katika uwanja wa power iso the uta save file yako as (.Iso) image utakuwa umebadilisha
ANDAA FLASH IWEZE KU BOOT KATIKA COMPUTER
Fuata hatua zifuazazo
Juu kabisa ya software nenda katika uwanja umeandikwa tools bofya hapo itakuja menu ina vitu vingi wewe utachagua create bootable Usb Drive itafunguka box hii hapa
Wakati huo umechomeka flash yako katika Computer hatua inayo fuata ni ku bofya mahali pameandikwa image source file mahali ulipo save image yako ya window itakuletea window zote zilizo katika mfumo wa image kama hivi
Chagua window unayo taka then Bonyeza Start Button Software itafanya kazi yake mpaka mwisho itakuambia ume fanikiwa sasa una weza ukaweka flash katika computer yoyote na kuweka wendow bila shida.
JINSI YA KUINSTALL WINDOW KATIKA COMPUTER YAKO BAADA YA KUANDAA FLASH.
Weka Flash yako katika computer alafu zima computer yako baada ya hapo washa ,kabla computer haijawaka press button F12 juu kabisa ya computer yako au minya escape
Baada ya hapo computer itakudai unataka kuboot toka wapi basi chagua mahali pa usb and flash drive uweze ku boot computer yako. Hapo window itafanya installation hadi mwisho kabisa na hatua zingine ni za kawaida tu kuset password pamoja na kuandika user name ya computer.