Zifatazo ni hatua za kufata, fuata hatua hizi kwa umakini na utafanikiwa bila shida
1. Zima simu yako toa betri na ulirudishe,
2. a) Kama unatumia HUAWEI,VODAFONE AU TECNO bonyeza button ya kuongezea sauti na ya kuwashia kwa pamoja kwa sekunde 15, kufanya hivyo kutakuletea Recovery menu.
b)kama unatumia Samsung bonyeza buttonya kuwashia, kuongezea sauti na home button kwa sekunde 15, kufanya hivyo kutakuletea Recovery menu.
3. Tumia button ya kupunguzia sauti na ushuke mpaka kwenye wipe data/factory reset
4. Bonyeza button ya kuwashia kisha tumia button ya kupunguzia sauti kushuka mpaka kwenye delete all users data then bonyeza button ya kuwashia. (kwa baadhi ya sim za tecno na Sony Bonyeza button ya kuongezea sauti kisha tumia button ya kupunguzia sauti kushuka mpaka kwenye delete all users data then bonyeza button ya kuongezea sauti)
5. Iache kwa muda kisha utaona neno Reboot now liko highlighted bonyeza button ya kuwashia kisha iache izime na iwake( kwa baadhi ya sim zitakuomba ukubali kufuta bonyeza button ya kuwashia kisha utaona neno Reboot now liko highlighted bonyeza button ya kuwashia kisha iache izime na iwake) kwa kesi ya baadhi ya simu utatumia button ya kuongezea sauti badala ya button ya kuwashia.
6. Hapo utakuwa umefanikiwa kuondoa pattern au password kwenye simu yako
MWISHO
denismyamba@2016
myambad@gmail.com
No comments:
Post a Comment