HOME

Thursday, 15 December 2016

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA COMPUTER

1. UKUBWA WA RAM
nendo ram ni kifup cha neno RANDOM ACCESS MEMORY. kazi kubwa ya RAM ni kuisaidia computer kufungua mafile na mafolder mbalimbali, pia hufihadhi taarifa kwa muda mfupi na taarifa hizi huwa zinafutika pale tu unapozima computer na kuwasha. ili computer iwe faster au iwe slow hutegemea sana ukubwa wa RAM. ndio maana RAM isipokuwepo kwenye computer yako haiwezi kuwaka, itaishia kuonesha charge inaingia lakini haiwaki.  kwahiyo unapotaka kununua computer hakikisha RAM inakuwa na ukubwa wa atleast 2GB

2. UKUBWA WA PROCESSOR
Processor ni kama ubongo wa computer yako, kitu chochote kinachofanyika kwenye computer processor ndio hufanya kazi hiyo. yan mfano unabonyeza herufi M na inatokea, kitendo hiki cha kubonyeza na kutokea huwa kinafanywa na PROCESSOR. kwa jina lingine processor huitwA CENTRAL PROCESSING UNIT. kwahiyo unapotaka kununua computer ni muhimu kuhakikisha processor yako inaukubwa kias, atleast kuanzia 2GB.

3. UKUBWA WA HARD DISK
hard diski ndio memory ya computer yako. humo ndio huhifadhiwa vitu vyote unavyoviweka kkwenye computer, mfano unapoweka mizki au movies au mafile yako yote huhifadhiwa kwenye HARD DISK, kwa kifupi huwa inaitwa HDD. ukubwa wa HDD hutegemeana na matumizi ya computer husika. kama unamatumizi makubwa computer yenye HDD kubwa. na kinyme chake ni sahihia nunua 

Saturday, 3 December 2016

JINSI YA KUBADILI PASSWORD KWENYE COMPUTER YAKO

Jinsi ya kubadili password kwenye computer yako fuata hatua zifuatazo.
(1)Washa computer yako ingiza password zako.
(2)Click kwa pamoja CTRL+ALT+DELETE.
(3)Utaona option nyingi wewe chagua "CHANGE PASSWORD".
(4)Ingiza old password(password unazotumia)
(5)Ingiza password mpya
(6)Confirm new password (hakikisha password mpya)
(7)Click button ya enter.
(8)hapo utakua umefanikisha kubadili password zako.

JINSI YA KUONDOA PATTERN AU LOCK KWENYE SIMU BILA KUFLASH NA BILA KUTUMIA SOFTWARE YOYOTE

Watu wengi wamekuwa wakipata tatizo la kusahau password au pattern kwenye simu zao, wengi huzani kwamba njia pekee ya kuiondoa hii ni kuflash simu, leo nitakwenda kufundisha njia rahis ya kuziondoa password bila kuiflash au bila software yoyote. Kwenye somo la leo nitatumia simu aina 4, ila hata kwenye simu nyingine njia hizi hutumika, nitatumia TECNO,HUAWEI,VODAFONE, na SAMSUNG.
Zifatazo ni hatua za kufata, fuata hatua hizi kwa umakini na utafanikiwa bila shida
 1. Zima simu yako toa betri na ulirudishe,
 2. a) Kama unatumia HUAWEI,VODAFONE AU TECNO bonyeza button ya kuongezea sauti na ya kuwashia kwa pamoja kwa sekunde 15, kufanya hivyo kutakuletea Recovery menu.
b)kama unatumia Samsung bonyeza buttonya kuwashia, kuongezea sauti na home button kwa sekunde 15, kufanya hivyo kutakuletea Recovery menu.
3. Tumia button ya kupunguzia sauti na ushuke mpaka kwenye wipe data/factory reset
4. Bonyeza button ya kuwashia kisha tumia button ya kupunguzia sauti kushuka mpaka kwenye delete all users data then bonyeza button ya kuwashia. (kwa baadhi ya sim za tecno na Sony Bonyeza button ya kuongezea sauti kisha tumia button ya kupunguzia sauti kushuka mpaka kwenye delete all users data then bonyeza button ya kuongezea sauti)
 5. Iache kwa muda kisha utaona neno Reboot now liko highlighted bonyeza button ya kuwashia kisha iache izime na iwake( kwa baadhi ya sim zitakuomba ukubali kufuta bonyeza button ya kuwashia kisha utaona neno Reboot now liko highlighted bonyeza button ya kuwashia kisha iache izime na iwake) kwa kesi ya baadhi ya simu utatumia button ya kuongezea sauti badala ya button ya kuwashia.
 6. Hapo utakuwa umefanikiwa kuondoa pattern au password kwenye simu yako
MWISHO
denismyamba@2016
myambad@gmail.com 

Thursday, 19 May 2016

JINSI YA KUTUMA FILES,DOCUMENTS,PROGRAMS KWA KUTUMIA WHATSAPP


Leo katika DARASA HURIA tutajifunza jinsi ya kutuma mafile au mafolder ambayo sio audio au video kwa kutumia whatsaap. Hii itakuwa msaada kwa wale miokuwa mnatamani kutumiana softwares au notes au documents mbalimbali kwa njia ya whatsaap. KARIBU
Whatsapp ni app ambayo imekuwa ikitumika na watu wengi kweny kutuma na kupokea audio na video, ni app inayopendwa na watu wengi sana kutokana na urahisi wake wa kutumia. Pamoja na kukuwezesha kushare files za multimedia(music, photos, video) lakini kuna kasoro iliyopo katika app hii. Nayo ni kwamba Haina uwezo wa kutuma files zilizopo katika mfumo wa software kama .exe, .apk, .bar n.k na pia files katika mfumo wa document (.docx, .pptx, .epub). Zipo njia baadhi zinazokuwezesha kutuma na kupokea mafaili ya mfumo huo, moja ya njia ambayo nadhani inafaa zaidi ni kwa kutumia programu ya kando(third party app) inayoitwa WhatsApp File Sender. Kupitia WhatsApp File Sender unaweza kutuma mafaili kama hati za kiofisi(office documents) (.doc, .docx, pptx), pdf, .epub na kadhalika. Si hayo tu, kwa kifupi unaweza kutuma na kupokea kila aina ya faili kwa WhatsApp kupitia programu hii, hata programu kama .exe (executable), .zip na .apk au chochote kile unachotaka.
JINSI YA KUTUMA FILES
STEPS.
1.Nenda kweny playstore na udownload  Whatsapp File Sender
2. Fungua WhatsApp File Sender, kisha angalia sehem wameandika SELECT FILE au chagua mafile utakayayaona chini ya hio neon SELECT FILE.
3. Tafuta faili unalotaka kutuma, kisha SEND
4. itakupeleka kwenye whatsapp account yako
5. Chagua unaemtumia kisha bonyeza "OK".
NAMNA YA KUPOKEA FAILI
STEPS
1. Download faili kwa WhatsApp yako ya kawaida
2. Baada tu ya kudownload, WhatsApp File Sender itafunguka yenyewe na kuomba ruhusa yako ili kufungua faili hilo (decode).
3. Elekeza sehemu unayotaka kuhifadhi hilo faili, unaweza tengeneza folder lake maalum kwa ajli tu ya kupokea mafaili kwa njia hii.
4. Kisha bonyeza Ok.

NOTE
Ili kufanikisha swala hili ni Lazima wote (mtumaji & mpokeaji ) wawe na WHATSAPP FILE SENDER (WTS)
WhatsApp File Sender hubadili mafaili (encoding) kwenda kwenye mfumo wa sauti (audio), na wakati wa kupokea hurudisha katika mfumo wake
wa kawaida (decoding).
Kwa Kawaida WhatsApp hutuma faili lisilozidi ukubwa wa MB 16, lakini kwa njia hii unaweza
kutuma faili lenye ukubwa wowote zaidi ya MB16.
Unaweza tuma vitu vingi kwa mara moja, tengeneza folder la ".zip" weka mafaili yote ndani yake, kisha tuma.
WhatsApp File Sender hugawa mafaili makubwa katika ukubwa wa MB 16 kila moja, hii
huwezesha kutuma mafaili makubwa zaidi.
Mpokeaji ni lazima ahakikishe vipande vyote vimefanikiwa kuwa downloaded kabla ya
decoding.
Hii ni Njia nzuri kwa makundi ya WhatsApp kutumiana mafaili ya kiofisi kama notes na mengineyo kwa urahisi zaidi